Psalms 47

Mtawala Mwenye Enzi Yote

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora.

1 aPigeni makofi, enyi mataifa yote,
mpigieni Mungu kelele za shangwe!
2 bJinsi gani alivyo wa kutisha, Bwana Aliye Juu Sana,
Mfalme mkuu juu ya dunia yote!
3 cAmetiisha mataifa chini yetu
watu wengi chini ya miguu yetu.
4 dAlituchagulia urithi wetu,
fahari ya Yakobo, aliyempenda.

5 eMungu amepaa kwa kelele za shangwe,
Bwana kwa sauti za tarumbeta.
6 fMwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa,
mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa.

7 gKwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote,
mwimbieni zaburi za sifa.
8 hMungu anatawala juu ya mataifa,
Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu.
9 iWakuu wa mataifa wanakusanyika
kama watu wa Mungu wa Abrahamu,
kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu;
yeye ametukuka sana.
Copyright information for SwhNEN